Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti Baraza la Chadema afunguka baada ya kuachiwa kwa dhamana

Chademapicc Data Hashimu Issa akiwa katika harakati zake za kisiasa

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema (Bazecha), Hashimu Issa (63) amesema alijua hakuwa na kesi ya msingi kutokana na waliomfungulia kesi hiyo ya jinai kushindwa kuiendesha.

Issa alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo na kuzisambaza kwenye mtandao wa YouTube, katika kesi namba 179/2021.

Issa alikamatwa jana Jumatano Februari 23, 2022 na polisi muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumfutia kesi ya jinai.

Baada ya kukamatwa alipelekwa Oysterbay kisha kituo kikuu cha Polisi alikoachiwa kwa dhamana.

Akizungumza baada ya kuachiwa,  Issa amesema tangu mwanzo alijua hakuna kesi ya msingi kutokana na waliomfungulia kesi kushindwa kuiendesha.

Amesema tangu kesi hiyo ifunguliwe Julai mwaka 2021  wamekuwa wakienda mahakamani bila kesi kuendelea.

“Cha kushangaza hata leo (jana) baada ya hakimu kuifuta wakati natoka nje ya chumba cha mahakama askari alinikamata na kuniweka chini ya ulinzi."

“Walinipeleka kituoni lakini badaye walipokuja mawakili wangu pamoja na viongozi wa chama waliniachia kwa dhamana bila kunieleza kosa langu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live