Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenisongole afuta kauli 'Mawaziri kuuza sura'

Mwenisongole Kauli.png Mbunge wa Mbozi George Mwenisongole

Thu, 2 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka bungeni Dodoma Mbunge wa Mbozi George Mwenisongole amelazimika kufuta kauli yake ya 'kuuza sura' baada ya baadhi Wabunge wanawake kuiita kauli hiyo ni ya kuudhi na ni ya matusi.

Katika kauli hiyo Mwenisongole amesema baadhi ya Mawaziri waliopeleka Wake zao wakati wakiwasilisha Bajeti za Wizara zao kwamba walikwenda kuuza sura Bungeni huku akitoa sifa kwa Waziri wa Nishati, January Makamba ambaye hajampeleka Mke wake kwamba yupo makini na hana mambo ya kuuza sura.

Kauli ya Mbunge Mwenisongole ikawasimamisha Wabunge Ruth Mayenga na Ester Matiko na kutoa taarifa wakimtaka Mbunge huyo kufuta kauli yake kwani inawadhalilisha Wanawake.

Ombi hilo lilikubaliwa na Mwenyekiti wa Bunge ndipo akamtaka Mbunge huyo kufuta kauli yake ndipo aendelee na mchango wake kwenye hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Nishati mwaka 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live