Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambe ahoji kauli ya Rais kuhusu mchakato, upembuzi yakinifu

57126 Pic+liwale

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Ndanda (CCM), Cecil Mwambe, amehoji ni kwa nini Serikali imekiuka maagizo ya Rais John Magufuli katika utekelezaji miradi mingi ikiwamo maji.

Mwambe alitoa kauli hiyo bungeni leo Jumatatu Mei 13, 2019 alipouliza kuhusu kukwama miradi ya maji katika maeneo mengi.

"Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ni miongoni mwa vitu ambavyo mheshimiwa Rais John Magufuli alivikataa mwaka 2015 akizindua Bunge hili, kwamba vinachelewesha utekelezaji. Je, kwa nini Serikali inaendelea na utaratibu huo," amehoji Mwambe.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Lathifah Chande, ametaka kujua ni lini mradi wa maji wa Liwale uliofanyiwa usanifu utaanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Pia, Chande ametaka kujua kata zitakazonufaika katika Wilaya ya Liwale.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema upembuzi na usanifu wa kina hufanyika kwa lengo la kujua thamani halisi za mradi hivyo hakuna madhara.

Habari zinazohusiana na hii

Kuhusu Liwale, amesema Serikali inatambua changamoto ya hali ya upatikanaji maji katika mji huo na tayari inatekeleza mpango wa muda mrefu na muda mfupi.

"Kwa upande wa muda mfupi, katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali imekamilisha mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika mji wa Liwale," amesema Aweso.

Amesema tayari kazi mbalimbali zimefanyika ikiwamo ukarabati wa kituo cha kusukuma maji, ununuzi na ulazaji mabomba umbali wa kilomita 16 na ununuzi wa dira za maji 200 kwa gharama ya Sh264 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz