Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu: Sheria inatumika kuvidhofisha

30831 Salum+pic TanzaniaWeb

Mon, 10 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar, Salum Mwalimu amesema muswada wa marekebisho wa vyama vya siasa uliosomwa bungeni Novemba 16 utaliliweka Taifa katika hatari kubwa kwa sababu utavuruga vyama vya siasa pamoja na maisha ya wananchi. Amesema hayo leo Desemba 9  katika mkutano uliovikutanishwa vyama 15 vya siasa vya upinzani wakati vikitoa tamko  lao linalopinga muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa uliosomwa bungeni Novemba 16 mwaka huu. Akizungumza katika mkutano huo Mwalimu amesema muswada hupo umelenga kuviua vyama vya upinzani baada ya kushindwa kupitia kuwarubuni madiwani na hivi sasa wanataka kutumia sheria. “Yaani leo hii tukitaka kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vyetu tukaombe kibali kwa msajili wa vyama vya siasa tena tuwaambie tunawafundisha nini, nani kadhamini na kwa muda gani huu ni wendawazimu,” Amesema suala hilo linalenga kudhoofisha ushiriki wa wabunge wa upinzani wawapo bungeni washindwe kufanya jambo lolote. Amesema pia suala la kumtaka msajili kutaka taarifa yoyote ya chama kutoka kwa mtu yoyote unalenga kuvigombanisha vyama.  “Kama wanayoyafanya ni mema kwa nini wawekewe kinga ya kutoshitakiwa na kwa sababu kapewa nguvu ya kuviagiza vyama vya siasa kufanya marekebisho ndani ya miezi sita juu ya jambo lolote wanaweza siku kutuambia hawataki tuwe na makatibu wakuu. “Na huyu anaweza kutuamuru tuondoe vifungu vya msingi katika katiba zetu ili waweze kutudhofisha, sisi tutasema hapana. “Sheria ya kusema chama kitakachopata ripoti isiyoridhisha kizuiliwa ruzuku kwa miezi sita ni jambo gumu kwa sababu tangu awali tulikuwa tukimpinga  na hivi sasa ameamua kujipa kinga ili afanye mambo kwa mujibu wa sheria,” amesema Mwalimu. Amesema pia mamlaka ya kumvua uanachama mtu yoyote haujalenga wananchi bali watu walio na ushawishi ndani ya vyama pamoja na viongozi wakubwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz