Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwaipaya wa Chadema aachiwa

Mwaipaya Pic Data Mwaipaya wa Chadema aachiwa

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya ameachiwakwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano.

Taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Morogoro, Jackson Malisa ilieleza kuwa Mwaipaya alikamatwa Alhamisi Juni 30 saa 10 jioni akiwa eneo la Tarminal Pub Msamvu.

Alisema baada ya kukamatwa, uongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro ulienda Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro ambapo walipewa maelezo kuwa Mwaipaya amekamatwa kwa maelekezo ya jeshi hilo mkoa wa Dodoma na siku inayofuata (Ijumaa) angepelekwa Dodoma.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa jana Jumanne Julai 5, 2022 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano-Bavicha, Apolinary Boniface imeeleza kuwa Mwaipaya amedhaminiwa na watu wawili kwa masharti ya kuripoti kituoni hapo Julai 8.

Baada ya viongozi wa chama hicho kupata taarifa ya kukamatwa Ijumaa na Jumamosi, Mwaipaya hakuonekana Dodoma wala Morogoro na kuzua wasiwasi kwa familia, ndugu na chama kutoonekana kwake.

Taarifaya iliyotolewa na Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika ilieleza kuwa chama kimechukua hatua kwa kuwasilisha Habeas Corpus Mahakama Kuu Dodoma dhidi ya Polisi kumshikilia Mwaipaya kinyume na sheria na kutaka apewe dhamana au kufikishwa Mahakamani.

Advertisement Hata hivyo leo, kesi ya maombi madogo ya jinai inayowakabili Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Kamanda wa Polisi (RPC) na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) Dodoma iliahirishwa baada ya washtakiwa hao kutofika mahakamani.

Katika shauri hilo la maombi madogo ya jinai namba 25/2022, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiliiomba Mahakama Kuu kutoa amri ya kuachiwa kwa Mwaipaya.

Akizungumza nje ya mahakama, Wakili wa upande wa mashtaka, Fredrick Kalonga alidai kuwa Jaji Dk Adam Mambi amefanya busara kuahirisha kesi hiyo hadi zitakapokwenda mahakamani pande zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live