Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua yaahirisha mkutano wa Chadema Mbeya

Chadema 841598 Maandamano Chadema.

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliokuwa unafanyika kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe, umeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha. 

Tukio hilo limetokea leo Jumanne, tarehe 20 Februari 2024, jijini Mbeya, baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kuuahirisha muda mfupi baada ya mkutano huo kuanza ambapo viongozi wakuu wa chama hicho walikuwa hawajaanza kuzungumza.

Mkutano huo ulifanyika baada ya Chadema kufanya maandamano kuanzia asubuhi ya leo, ambapo ilipanga kuyahitimisha kwa kufanya mkutano huo wa hadhara.

“Kazi kubwa iliyotuleta Mbeya leo ilikuwa ni maandamano, kazi ambayo tumeimaliza ahsanteni sana, kwa hali ya hewa ilivyo na kwa namna ambavyo wanaharibiwa kamera zao wanahabari wetu ni naomba kwa leo tumshukuru Mungu angalau yameweza kutoka Mbalizi na Uyole mpaka hapa, hiyo ni Baraka kubwa sana kwa Mungu,” amesema Mbowe na kuongeza

“Kwa maana hiyo mkutano wetu wa hadhara kwa siku ya leo hautaendelea, tutatangaza tarehe mpya ya siku nyingine tutazungumza kwa muda mrefu.”

Awali, watu kadhaa walipata nafasi ya kuzumza akiwemo  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, aliyesema ameunga mkono maandamano hayo ili kudai katiba mpya na kuishinikiza serikali itatue changamoto ya ugumu wa maisha.

“Katiba ya leo tuliyo nayo tunaita katiba ya 1977 ilitengenezw a na watuw asiozidi 20 kwa siku chache, hakuna sababu leo Samia na Serikali yake kutuambia muda hautoshi tunataka kumwambia Samia, katiba ni mali ya watanzania kama alichaguliwa kwa mujibu wa katiba lazima aiheshimu na kuitii katiba. Tunaungana na Chadema na tutaungana na asasi na wale wanaopigania kupunguza gharama za maisha na wanaopambana tupate katiba mpya,” amesema Slaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live