Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musukuma kutumia chopa kukomboa kata Arusha

10526 Pic+musukuma TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (CCM) maarufu ‘Musukuma’ ameahidi ataanza kutumia chopa katika wiki hii ya mwisho ya kampeni ili kuhakikisha kata zote za Monduli na Arusha Mjini zinarudi CCM.

Akizungumza katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani katika Kata ya Migungani wilayani Monduli, Benedict Mawala, Musukuma alisema amepanga kuhakikisha CCM inashinda kata zote.

“Kuanzia wiki ijayo nitakuja na chopa tutakuwa na Kalanga (aliyekuwa mbunge wa Chadema jimbo la Monduli), tutaruka na kufanya mikutano,” alisema.

Musukuma aliwataka wakazi wa kata hiyo, kutofanya makosa tena kwa kuchagua madiwani wa Chadema.

Alisema Mawala ambaye alitimkia Chadema mwaka 2015 sawa na aliyekuwa mbunge, Kalanga, sasa wamejua ukweli na wamerejea CCM kwa baba yao kwa kuwa mtoto hafukuzwi nyumbani.

“Wamegundua kule ni Saccos siyo chama siasa, wamerudi kwenye chama chao, tuwapokee na kuwaunga mkono,” alisema

Mawala aliomba wakazi wa kata hiyo kumchagua tena kuwa diwani kwa kuwa ni amerejea CCM, chama chenye Serikali.

“Nimerudi nyumbani naomba mnichague nitashirikiana na serikali kuwaletea maendeleo yenu yote niliyoahidi wakati ule nikiwa upinzani sasa nitatekeleza kwa kushirikiana na serikali,” alisema.

Katika jimbo la Monduli utafanyika uchaguzi katika kata tatu baada ya wagombea wengine watatu wa CCM kupita bila kupingwa.

Katika jimbo la Arusha lenye upinzani uchaguzi utafanyika kwenye kata nne ambapo CCM yenye wagombea waliojiuzulu udiwani Chadema inachuana tena na chama hicho kikuu cha upinzani.

Chanzo: mwananchi.co.tz