Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musukuma aahidi Mto wa Mbu kuwa mamlaka ya mji mdogo

15086 Msukuma+pic TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Musukuma’ amewataka wakazi wa kata ya Mto wa Mbu kumchagua Julius Kalanga kuwa mbunge wa Monduli ili eneo hilo kupata hadhi ya kuwa mamlaka ya mji mdogo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za uchaguzi zilizofanyika katika kata hiyo leo Jumamosi Septemba Mosi, 2018, Musukuma amesema Mto wa Mbu ina sifa ya kuwa mji mdogo.

“Mchagueni Kalanga tutashirikiana nae ili hapa pawe  mamlaka ya mji mdogo, kwani mnakosa nini,” amesema na kuwataka mamia ya wananchi waliojitokeza  kubadilika kwa kuwa sasa Kalanga anagombea akiwa CCM.

Kalanga alikuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya Chadema kuanzia 2015 hadi Julai 31, 2018 alipohamia  CCM ambako amepitishwa kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

Kwa upande wake Kalanga amesema anajua shida za Mto wa Mbu na hata kabla ya kujiunga na CCM alikuwa akifika kuwasikiliza wananchi.

Amesema  wakimchagua atahakikisha eneo hilo linakuwa na stendi ya mabasi na soko la kisasa la ndizi.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz