Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musukuma: Kalanga ataipatia Mto wa Mbu mamlaka ya mji

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma amewataka wakazi wa Mto wa Mbu mkoani Arusha kumchagua mgombea wa ubunge wa CCM, Julius Kalanga kwa kuwa atahakikisha eneo hilo linapata hadhi ya mamlaka ya Mji Mdogo.

Akizungumza kwenye kampeni za kumnadi Kalanga, Msukuma alisema Mto wa Mbu haistahili kuwa kata, ina sifa ya kuwa mji mdogo.

“Mchagueni Kalanga tutashirikiana naye wabunge tulio wengi kuomba hapa pawe Mamlaka ya mji mdogo kwani mnakosa nini,” alisema.

Aliwataka wakazi wa Mto wa Mbu kutopoteza fursa ya kubadilika sasa kutokana na kumpata Kalanga akitokea CCM.

Kwa upande wake Kalanga alisisitiza anajua shida za Mto wa Mbu na hata kabla ya kujiunga na CCM alikuwa akifika kuwasikiliza na akaahidi kuwasaidia kuwa na stendi ya mabasi na soko la kisasa la ndizi.

Kalanga aliyekuwa mbunge wa Monduli kupitia Chadema akijiuzulu na kujinga na CCM ambayo imesimamisha tena kuwania nafasi hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz