Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muro atumia mkutano wa kampeni kuzuia karoti kutoka nje

10514 Pic+muro TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Muro ametumia mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa CCM katika Kata ya Songoro kutangaza neema kwa wakulima wa karoti wilayani humo.

Katika mkutano huo, Muro alimnadi mgombea huyo, Charles Nko huku akipiga marufuku mazao ya karoti kutoka nje ya nchi kuingia wilayani Arumeru ili kulinda soko la wakulima wa ndani ya wilaya hiyo.

Akizungumza katika viwanja vya Sura ndani ya kata ya Songoro, Muro alisema kuanzia msimu ujao wa zao hilo unaotarajia kuanza Oktoba mwaka huu ni marufuku karoti kutoka nje ya nchi kuingia wilaya yake.

Katika mkutano huo, Muro alikuwa ameambatana na mbunge wa Longido mkoani hapa, Dk Stephen Kiruswa na mwenyekiti wa CCM wilayani Meru, Furahini Mungure.

Muro aliwaambia wanachama wa CCM kuwa hakutumwa na Rais kwa bahati mbaya na kuonya kuwa yoyote atakayekwamisha shughuli za maendeleo wilayani humo atakula naye sahani moja.

Nko aliwaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo huku akisema kwamba safari hii amerudi nyumbani kushirikiana na serikali kuwaletea maendeleo ya uhakika badala ya porojo.

(Moses Mashalla)

Chanzo: mwananchi.co.tz