Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muda waongezwa uboreshaji Daftari wapiga kura Dar

96475 Nec+pic Muda waongezwa uboreshaji Daftari wapiga kura Dar

Thu, 20 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (Nec) imeongeza muda wa siku tatu katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura Mkoa wa Dar es Salaam uliotarajiwa kufikia ukomo wake leo Alhamisi Februari 20, 2020.

Uboreshaji huo ulianza Februari 14 na leo ndio ilikuwa siku ya mwisho lakini tume hiyo imeongeza siku nyingine tatu mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 15(1) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura namba 343 pamoja na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura namba 292

"Kwa hiyo Ikifika tarehe 23, 2020  siku ya Jumapili hatutaongeza muda tena," amesema Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo, Dk Wilson Charles.

Katika ufafanuzi wake, Dk Charles amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia vyema muda huo.

Kwa mujibu wa tume hiyo, vituo 37,814 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo kwa Tanzania bara na visiwani.

 

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz