Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Odinga ashangazwa na baba yake kushindwa Urais

Winnie Odinga Mtoto wa Odinga ashangazwa na baba yake kushindwa Urais

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winnie Odinga ambaye ni kitinda mimba wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amesikitishwa na jinsi baba yake alivyokosa kutwaa ushindi wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Wakati aliporejea kwenye Twitter tangu aondoke mwezi Septemba, Winnie alisema wakati kama huu angekuwa yuko Ikulu na baba yake, ikiwa yeye ndiye angesimamia uchaguzi.

“Nimerudi Twitter baada ya muda, na kweli nimetupiwa makombora makali. Naona mmekuwa mkiongea sana.

"Jueni kwamba kuna tofauti kubwa ya kimfumo kati ya wakati wa kampeni za uchaguzi na siku ya uchaguzi. Kama ningesimamia uchaguzi, ningekuwa niko Ikulu saa hii.” Winnie alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live