Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtolea apita bila kupingwa Temeke

32619 Mtoleapic Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Abdallah Mtolea, aliyepitishwa na CCM kuwania Ubunge wa Temeke,  leo Alhamisi Desemba 20, 2018 amepita bila kupingwa baada ya wagombea waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo  kukosa sifa.

Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mtolea amekiri kupita bila kupingwa.

Katika hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge ambayo Mwananchi imeiona inaeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 81 (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, Mtolea amechaguliwa kuwa mbunge wa Temeke katika uchaguzi uliofanyika leo.

Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 



Chanzo: mwananchi.co.tz