Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtemvu aonya rushwa uchaguzi CCM

Mtemvu Ccm Dar G Abbas Mtemvu

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ameonya tabia ya kuchukua au kutoa rushwa kwenye kipindi hiki cha uchaguzi.

Alisema hayo alipokuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2021/2022 Kata ya Kivukoni, iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule.

Mtemvu amesema haiwezekani kuendelea kupitisha viongozi, wakiwamo madiwani na wabunge kwa kutoa rushwa. Alisema katika uongozi wake, hilo halitatokea.

“Katika nafasi yangu hii ya Mwenyekiti mliyonipa kwa kura nyingi, nisingependa kuona diwani ama mbunge anatoa rushwa.

Sitomvumilia kwa lolote lile, nitamuadabisha kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo ndani ya Chama,” amesema.

Akiongeza kuwa: “Unaweza kutoa au kupokea rushwa lakini mkaambulia kupata kiongozi mbovu asiyeweza kufanya kazi kwenye kata au jimbo.”

Amewataka wana CCM wa Dar es Salaam kuwa na umoja na mshikamano ili ifikapo mwaka 2025, mkoa utoe kura nyingi kwa Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kushika nafasi hiyo kwa miaka mingine.

Diwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule alimpongeza Mtemvu kwa kuchaguliwa na kumweleza kuwa kata yake imefanya mambo mengi ya kimaendeleo ila ina changamoto ya ofisi ya kudumu.

Mtemvu alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kushughulikia suala la upatikanaji wa ofisi ya Kata ya Kivukoni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live