Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtemvu aanza na kukemea makundi, rushwa

WhatsApp Image 2022 12 01 At 9.jpeg Mtemvu aanza na kukemea makundi, rushwa

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amesema hataki makundi, rushwa wala kukatana kwenye Mkoa wa Dar es Salama na kuwataka wanachama wote wa chama hicho wavunje makundi yao.

Mtevu ameyasema hayo Desemba Mosi, 2022 wakati akikabidhiwa ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam huku akieleza kwamba kazi yake ya kwanza ni kurudisha mshikamano, kurudisha matumaini kwa watu ambao wanasema wao wabaya.

“Kuna watu ilikuwa wanasema wakina Mtevu wabaya, tunataka kuwaonyesha kuwa sisi sio wabaya, tunachotaka ni umoja na mshikamano, Dar es Salaam imezidi kwa migogoro, sitapenda kuona mnagombana.

“Uchaguzi umeisha makundi mvunje, sisi sote ni kitu kimoja, haina maana kugombana, na watakaoendeleza migogoro tutafungia, na msikimbilie msituni tukae humu humu kama kuonyana tuonyane.Watakaobainika kula rushwa tutawafungia, tunataka Dar iliyo safi, na nikikufungia mimi hakuna wa kukufungulia," amesema.

Aidha, Mtevu amesema hakutarajia kushinda kwa kura za kishindo na kuwashukuru wanachama wa CCM Dar es Salaam kwa kumchagua.

“Nimepata kura 440 nilijua nitashinda, lakini sikujua kama nitashinda kwa kishindo, nilijua nitashinda kutokana na timu nilizokuwa napambana nazo, nilijua nitashinda ila si kwa mabao mengi hivi…;

“Kila ninavyokaa nafikiria nitaifanyia nini CCM Dar es Salaam.”

Kwa upande wa Mwenyekiti Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa kura za ndio huku akiahidi pia ushirikiano kwa wanachama na viongozi wote wa mkoa wa Dar es Salaam katika kutekeleza ilani ya CCM.

Amesema katika chaguzi makundi hayaepukiki ila baadaye yanakwisha baada ya uchaguzi kumalizika na kuwa wamoja kukijenga na kukiimarisha Chama.

Amesema jukumu lao kubwa kama viongozi waliochaguliwa ni kuyaunganisha makundi yote, ukizingatia kuwa chaguzi hizo ni za ndani ya chama huwa wanajipanga na siyo kushindana na kwamba umoja, mshikamano miongoni mwa wanachama ndio nguzo imara.

Kwa kukumbusha tu, Mtevu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 444 katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni na kumwangusha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mama Kate Kamba aliyepata kura 160.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live