Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msukuma awaonya Chadema kutumia jina lake kutafuta umaarufu

Msukuma Kiba.jpeg Msukuma awaonya Chadema kutumia jina lake kutafuta umaarufu

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa jimbo la Geita, Joseph Kasheku 'Msukuma' amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kuacha kutumia jina lake kwa ajili ya upotoshaji juu ya uwekezaji unaotaka kufanywa na serikali.

Msukuma ameyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyawilimilwa wilayani Geita.

Anasema kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakikusanya watu kwenye mikutano yao kwa kupitia jina lake hivyo waache mara moja.

“Unajenga treni ya kisasa kutoka Dar mpaka Mwanza, tumejengewa Daraja la Busisi, fela, sasa unatengeneza hayo mazuri ili upitishe nini? Wewe unapitisha mizigo tani milioni 18, treni unayojenga itabeba tani milioni 25 kwa mwaka, maana yake haitapata mizigo na malori yako yatalala.

“Wamekuja huku wamesema sisi ni wajinga, waambieni sisi sio wajinga, wanasema Bandari ya Senga, Mharamba na Nkome zimeuzwa, kuna mzungu wa kuja kuishi Senga ambako kuna mitumbwi mitatu tu? Mlishawahi kuona meli inashusha mizigo hapo? Hakuna mtu ambaye atauza nchi yake.

“Nimeingia halmashauri nikakuta tunalipwa Tsh milioni 400 kwa mwaka, nikapambana tukafanya vurugu, tukaandamana, tukalala lockup, tukamshinda kesi na leo tunalipwa Tsh bilioni 18 kwa mwaka. Ningetaka rushwa si ningekula za wazungu hapa, tena hazina hata kele wala msingejua.

“Kwa sababu mimi ni maarufu lazima watumie jina la Msukuma ili wajitangaze kimataifa, hivi vitu vipo tu. Mimi ni maarufu ukichukua wabunge 10 na mimi nimo, unadhani mchezo. Nyie watu wa upinzani mliohamia hapa Nyamwilimilwa fuateni kilichowaleta,” amesema Msukuma.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela anasema miundombinu ya barabara na bandari ikikamilika itasaidia wakulima kusafirisha mazao yao nchi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita Nickolous Kasendamila amewaomba wananchi kuacha kusikiliza maneno ya upotoshaji kwa CCM, ndio chama kinachojali changamoto zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live