Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Msivae tai nyekundu leo Rais akija Bungeni" Ndugai

Red 660x400.jpeg "Msivae tai nyekundu leo Rais akija Bungeni" Ndugai

Thu, 22 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewataka wabunge kuzingatia itifakia hususani katika uvaaji bungeni, ambapo amewashauri waheshimiwa wabunge kutokuvaa tai nyekundu.

Ndugai amesema hayo mara baada ya kuhitimisha kipindi cha maswali na majibu bungeni leo, ambapo amesema anapokuja kiongozi hususani mkuu wa nchi haishauriwi mtu mwingine kuvaa tai nyekundu.   “Ningependa kuwakumbusha ndugu wabunge siku anayokuja kiongozi mkuu wa nchi basi haishauriwi sana kwa wenzangu mimi kuvaa tai nyekundu, nadhani tumekubali ile red inabakia na mwenye mamalaka, ni vizuri kuyajua hayo mambo jioni tutakaporudi na tai nyekundu utarudia geti la nje,” Ndugai.

Alasiri ya leo tarehe 22/04/2021 majira ya saa kumi jioni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kulihutubia bunge pamoja na kutoa mwongozo wa serikali yake ya  awamu ya sita, bungeni Dodoma.

Chanzo: millardayo.com