Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamo wa CHADEMA kongamano TCD

Mbowepic Siasa Leo Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama ha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetoa msimamo wa kushiriki katika kongamano la vyama vya siasa linatoratibiwa na Kituo cha Demokrasia nchini TCD, kuwa hawatashiriki kongamano hilo kwani kimsingi halikidhi matakwa ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 18, 2022 Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Aikael Mbowe amesema kuwa kongamano hilo halijalenga kujadili kuhusu katiba mpya na kwasasa hitaji kubwa la wananchi ni uwepo wa katiba mpya.

Awali kabla ya Mwenyekiti huyo kuachiwa huru, Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis S. Mutungi aliitisha mkutano wa vyama vya siasa ambapo CHADEMA waligoma kushiriki mkutano huo kwa madai ya ukiukwaji wa haki za msingi ikiwemo kushikiliwa kwa kiongozi huyo.

Mbowe akirejelea hilo amesema kuwa chama hicho kimeumizwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni maridhiano ambayo yatajumuisha upatikanaji wa Katiba mpya.

"Tumekubaliana kama CHADEMA tutashiriki mazungumzo yote yenye nia njema , kongamano linalopangwa Dodoma kwa mtazamo wetu agenda yake haizungumzii katiba mpya bali inakwepa hoja ya katiba mpya,

"Nisema vilevile maridhiano hayafanywi na kikao kimoja ni muendelezo, sio mnakurupuana mnakwenda kwenye kongamano mnakaa dakika nane eti mmekubaliana hapana haipo hivyo"

Miongoni mwa wawasilishaji mada ni Mahela aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, huyo akatukalishe sisi atuhubirie maridhiano"

Pamoja na kusamehe tumesema kuwa tutangulize maridhiano tuone wapi tumejikwaa"

"Sisi tumeumizwa, wanaoshiriki huenda wao hawajaumizwa" amesema Mbowe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live