Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msigwa: CCM ‘itapata taabu sana’

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mbunge Wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa amesema endapo vyama vya siasa vitafutika hapa nchini basi watumishi wa Serekali na CCM ‘watapata tabu sana’.

Mchungaji Msigwa alisema hayo katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Mwangata Taifa, Samweli Ngasapa.

Uzinduzi huo pia uliudhudhuriwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama hicho Mkoa wa Iringa, Suzani Mgonakulima.

Chadema inaingia katika uchaguzi huu ikiwana imebakiwa na kata moja kati ya sita ambazo zimeshachukuliwa na CCM baada ya kubainika kuwa wagombea wa chama hicho kuenguliwa.

Msigwa alidai baadhi ya watumishi wa Serekali kwa kwa kushirikiana na CCM wamekuwa wakikihujumu chama hicho kwa lengo la kushinda uchaguzi.

Msigwa aliwatahadharisha watumishi hao kuacha, kwa kuwa hata wao hawatabaki salama.

Alisema kuwa licha ya CCM kuiba na kununua madiwani wao lakini chama hicho bado kimeendelea kutegemea Jeshi la Polisi na kuweka mpira kwapani kwa kupoka baadhi ya kata.

“Chama hakipo tayari kuiachia Halmashauri ya Manispaa na hatujasusa kushiriki uchaguzi katika kata moja iliyosalia; tumeingia katika uwanja wa mapambano na tunaamini ushindi upo kwetu,” alisema Msigwa.

“Wameshatufanyia figisufigisu na tayari wamepora kata tano kwa ujanja ujanja, maana CCM hawana ubavu wa kushindana katika majukwaa.

Alisema chama hicho kimewapandikiza watu wao wanaowahujumu lakini hilo haliwatishi kwa kuwa kwao ushindi ni lazima.

“CCM ni wepesi sana hawawezi siasa za majukwani, wamezoea wizi wa kura, matukio ya kuvunja haki kama kuwaweka ndani wanachama wetu na matuko ya kutuvuruga lakini hilo halitatukatisha tamaa,” alisisitiza Msigwa.

Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia chama hicho, Ngasapa aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua ili kupambana kufa na kupona kwa ajili ya kuwatumikia.

“Haitatokea mtu au kikundi chochote kitakachoweza kunishawishi kwa fedha kama ilivyotokea kwa waliyepita,” alisisitiza.

Ngasapa alisema kuwa Tanzania siyo masikini na imekuwa na bandari kubwa inayotegemewa na nchi nyingine lakini bado imeendelea kuwa maskini kutokana na uongozi wa CCM .

‘Mimi nimekuja kuwatumikia na ukitaka tufanikiwe tuiondoe CCM madarakani, sitamuogopa mtu, sitajibembeleza kwakuwa sina biashara ambayo itasababisha nisumbuliwe na mamlaka husika.

‘Ngasapa aliwaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua ili aweze kuwaletea maendelea ya kweli tofauti na ilivyo sasa.

Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema, Iringa Frank Nyalusi alisema nhakuna atakayekuwa salama kama Chadema haitakuwa salama.

Chanzo: mwananchi.co.tz