Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii Baba Levo kusuka au kunyoa leo

18104 Pic+babalevo TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Hatma ya diwani wa kata ya Mwanga (ACT-Wazalendo), Crayton Revocatus maarufu ‘Baba Levo’ anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia muuguzi itajulikana leo hukumu itakapotolewa mjini Kigoma.

Baba Levo ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mjini Kigoma leo kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili.

Diwani huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya kushambulia, vurugu na lugha ya matusi dhidi ya muuguzi wa zahanati ya Msufini, Christina Gervas.

Msanii huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 12 na shtaka hilo kusomwa kwa mara ya kwanza Mei 4.

Kesi hiyo namba 62 ya mwaka 2018 ilikuwa ikisikilizwa kwa Hakimu Mfawidhi Flora Mtalania, huku msanii huyo akitetewa na wakili Thomas Msasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz