Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili wa vyama atoa ujumbe, AAFP wachaguana

Aafp Pic Msajili wa vyama atoa ujumbe, AAFP wachaguana

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutengeneza sera za jinsia ili kuunga juhudi za Serikali na Kitaifa kukuza masuala ya jinsia na kujumuisha makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu.

Akizungumza hayo jana Jumapili Februari 12, 2023 Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema hayo katika mkutano mkuu wa Chama cha siasa cha Wakulima (AAFP) ambapo wamefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali.

Nyahoza amesema vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutengeneza sera ya jinsia ili kuleta usawa katika ngazi mbalimbali za uongozi kwa kuwashirikisha makundi ya watu wenye ulemavu.

Amesema kwa vyama ambavyo hawafanyi vizuri amevitaka kutimiza matakwa ya sheria na vitakaguliwa jinsi gani vinatekeleza sera ya jinsia kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.

"Kifungu cha 6 (a) cha sheria ya vyama vya siasa inasisitiza chama cha siasa lazima kiendeshwe kwa kuzingatia misingi ya jinsia na kujali makundi maalumu ya jamii ikiwemo ya watu wenye ulemavu,"amesema Nyahoza.

Pia, Nyahoza amevitaka vyama vya siasa kuheshimu misingi ya demokrasia wanapokuwa kwenye chaguzi za ndani na wasipoheshimu wakichaguliwa kwenye uongozi mbalimbali ikiwemo mwenyekiti wa serikali ya mtaa hadi ubunge watafanya vibaya katika utendaji wao wa kazi.

Naye Mwenyekiti wa AAFP aliyechaguliwa tena, Said Sound Said amesema wamepitisha sheria ya jinsia ili wanawake na watu wenye ulemavu wapate nafasi za uongozi mbalimbali kwa kuwa wapo wenye elimu ya shahada hadi udaktari lazima wafanye kazi.

Pia, ameiomba Serikali kupitia sheria ibara ya 9(I) kinasema utajiri wa nchi ututumika kuondoa maradhi, ujinga na umaskini hivyo utajiri huo utumike kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi.

Said amesema katika mikutano yao ya hadhara watakuwa na agenda ya kusisitiza katiba iliyopo ifanyiwe kazi kabla ya kupata katiba mpya.

"Tunaungana na vyama vingine vya siasa kupata katiba mpya lakini hatupingi katiba iliyopo tunachosisitiza ifanyiwe marekebisho kabla ya hiyo katiba mpya," amesema Said

Wakati huo huo Mwenyekiti wa uchaguzi, Dk Thomas Nagaikaya ametangaza uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa wa chama hicho ni Said Sound Said ametetea nafasi yake kwa kupata kura 112.

Amesema Makamu mwenyekiti Taifa upande wa Bara amechaguliwa Nacy Mrikaria amepata kura 110 huku Makamu Mwenyekiti Taifa upande wa Zanzibar ni Juma Said Omary amepata kura 113 ambao wote wametetea nafasi zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live