Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili asimamisha mikutano ya kisiasa

JAJI  MUTUNGIIIIII Msajili asimamisha mikutano ya kisiasa

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo

Chanzo: eatv.tv