Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili aonya vyama vya siasa nchini

5be68c07a7d2fe7071bfab50e07e973e Msajili aonya vyama vya siasa nchini

Thu, 6 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema vyama vinaweza kufanya mbwembwe zote lakini viheshimu sheria za nchi.

Aidha, vyama vya siasa vya upinzani nchini vimesema haviwezi kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila nguvu ya pamoja katika kusimamisha wagombea wakiwemo kuwa na mgombea mmoja Tanzania Bara na mmoja Zanzibar.

Vyama vya upinzani vilitoa kauli hiyo wakatii wa Mkutano Mkuu Maalumu wa ACT-Wazalendo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Viongozi wa kisiasa wakitoa salamu za vyama vyao wakati wa mkutano huo walisema wapo tayari kuweka nguvu ya pamoja katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, ili kuiondoa CCM madaraki na wakakiri kuwa, kama hawatashirikiana, wasahau ushindi. Makamu Mwenyekiti wa NCCRMageuzi, Haji Ambar alisema Katiba ya chama hicho inaeleza kuhusu ushirikiano wa vyama na kusisitiza kuwa, wapo tayari kwa hilo.

Mwakilishi wa Chauma, Mohamed Masoud Rashid alisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na kuvitaka vyama viungane. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salim Mwalimu alisema chama hicho kinaamimi vyama vya siasa vitakwenda kwenye kushirikiana na si kuungana.

“Kila mmoja anatambua umuhimu wa kushirikiana, kazi imeanza na naamini tutaimaliza salama na tupo tayari kwa ushirikiano,” alisema Mwalimu.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, Tundu Lissu alisema ikiwa CCM itashinda kwa haki, wataridhia, lakini ikiwa kwa dhuluma, wataingia barabarani.

Katika mkutano huo uliobeba ajenda kuu mbili ikiwemo ya uchaguzi wa wagombea urais na kutoa taarifa ya mchakato wa Ilani ya chama hicho, bara na visiwani, viongozi hao na wengine wa taasisi za dini na asasi za kiraia, walitaka katiba ya nchi ilindwe na kutaka taasisi za serikali zinazosimamia demokrasia nchini, zisimamie katiba.

Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba, Bob Chacha Wangwe alitaka vyama vishindane kwa hoja katika Uchaguzi Mkuu, viungane na kuheshimu katiba. Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, alisititia umuhimu wa kushirikiana.

Mwenyekiti wa chama hicho, Seif Sharif Hamad, akifungua mkutano huo, aliwataka wajumbe wahakikishe wanachagua watu wanaouzika kwa wananchi na kueleza kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana na vyama vingine.

Katika mkutano huo, Bernard Member alichaguliwa na kutangazwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho na Seif Sharif Hamad amechaguliwa na kutangazwa mgombea urais Zanzibar.

Chanzo: habarileo.co.tz