Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili 'amtuma' Lipumba kufikisha salamu zake upinzani

660ac15b3bba2160bd4e547a29ec104e Msajili 'amtuma' Lipumba kufikisha salamu zake upinzani

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya upinzani kuwa na utulivu mwaka huu wa 2021.

Jaji Mutungi aliyasema hayo leo katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yaliyofanyika viwanja vya Chinangali, Dodoma.

Mutungi alimtaka Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahimu Lipumba kuzungumza na wenzake kutoka

upinzani kuwa wazalendo.

“Profesa Ibrahim Lipumba, kawaambie wapinzani wenzako watulie, waache kutoka toka nje, wakae kwa kutulia hii ni 2021 na waache kuwasilisha masuala ya Bunge kukiwa na masuala ya Kitaifa, 2021 muwe wazalendo” alishauri.

Aidha Jaji Mutungi aliipa kongole idara ya Mahakama kwa kuaminika na wananchi na wanasiasa na kutaka vyama vya siasa kuacha kutumia mahakama kupandikiza kesi.

"Mimi kama msajili wa vyama vya siasa bila kigugumizi chochote ninaweza nikasema hata vyama vya siasa vimekuwa na imani kubwa na Mahakama zetu, ndiyo maana kila nikitoa maamuzi wanakimbilia Mahakama, ninachowaomba muendelee kuiamini," amesema Jaji Mutungi

Chanzo: habarileo.co.tz