Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili aipa CUF siku 8 kueleza sababu ya kufukuza makada wake 10

Cufpic Msajili aipa CUF siku 8 kueleza sababu ya kufukuza makada wake 10

Fri, 26 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amekipa CUF siku nane kuwasilisha maelezo kuhusu kuwafukuza na kuwasimamisha uanachama vigogo 10 wa chama hicho.

Novemba 9 mwaka huu, Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililoketi kati Novemba 5 na 6 lilitangaza kuwavua uanachama viongozi wake mbalimbali, akiwemo aliyewahi kuwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa CUF, Abdul Kambaya kwa tuhuma za kukihujumu chama hicho.

Wengine ni Chande Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya Vijana ya CUF (JUVICUF), Ali Makame Issa , Mtumwa Ambari Abdallah , Mohamed Vuai Makame na Dhifaa Bakari, Hamida Abdallah Haweshi ambao wote walikuwa wajumbe wa Baraza Kuu la CUF.

Waliopewa onyo kali la maandishi ni pamoja na Yasin Mrotwa, Ali Rashid Abarani, Masoud Ali Said, Said Omar na Mussa Haji Kombo aliyewahi kuwa kaimu makamu mwenyekiti wa CUF-Zanzibar. Huku aliyekuwa mwenyekiti wa JuviCUF Hamidu Bobali na Ahmed Salum Khamis wakiwekwa chini ya uangalizi wa miezi sita.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa jana na Naibu Msajili wa Vyama Siasa, Sisty Nyahoza kwa niaba ya Jaji Mutungi, kwenda ofisi ya katibu mkuu wa CUF, iliwataka chama hicho kuwasilisha malalamiko dhidi ya wanachama hao waliowafukuza huku wengine wakiwasimamisha ili msajili kujua kama yaliyowasilishwa na walalamikaji ni kweli au la.

“Maelezo yenu yawasilishwe ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Dodoma siyo Desemba 3 saa tisa na nusu mchana,” amesema Nyahoza.

Amefafanunua kuwa wanachama hao 10 wamewasilisha malalamiko yao kwa msajili kupinga uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF, wakidai wamepewa adhabu bila kuzingatia matakwa ya Katiba na kanuni za chama hicho.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 6a (2), 6a (2) na 5b ya Sheria ya Vyama vya Siasa’the political parties act CA 258 na kanuni ya 23 (1) ya kanuni political parties (registration and monitoring) regulation 2019, CUF –Chama cha Wananchi mnapaswa kuwasilisha maelezo hayo,” amesema Nyahoza katika barua hiyo.

Chanzo: mwananchidigital