Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msajili Vyama vya Siasa awaonya upinzani "2021 muwe wazalendo"

Mutungi 660x400 Msajili Vyama vya Siasa awaonya upinzani "2021 muwe wazalendo"

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amemuagiza Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, kwamba akawaambie wapinzani wenzake watulie na waache kuwasilisha masuala ya Bunge kukiwa na masuala ya Kitaifa na kwamba huu mwaka 2021 wawe na uzalendo.

“Mimi kama Msajili wa Vyama vya Siasa bila kigugumizi chochote ninaweza nikasema hata Vyama vya Siasa vimekuwa na imani kubwa na Mahakama zetu, ndiyo maana kila nikitoa maamuzi wanakimbilia Mahakama, ninachowaomba muendelee kuiamini” Jaji Mutungi

“Ndugu yangu Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Rais nimesikia anakuomba kuhusiana na Katiba nilijua lazima wanasiasa watakukumbushia, namuomba  Lipumba akawaambie wenzake ule mchezo wa kutoka toka kwenye Mabunge kukwamisha haya masuala muhimu ya kitaifa basi wayapunguze, 2021 tuwe ni watu wenye uzalendo tukiwa na masuala ya kitaifa mambo ya kuinuka inuka kutoka kwenye Bunge hayo tuyaache” Jaji Mutungi.

Chanzo: millardayo.com