Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msafara wa Biteko wakutana na maandamano ya Chadema, polisi watuliza hali ya hewa - VIDEO

Msafara Wa Biteko Wakutana Na Maandamano Ya Chadema, Polisi Watuliza Hali Ya Hewa Msafara wa Biteko wakutana na maandamano ya Chadema, polisi watuliza hali ya hewa

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko umekutana na msafara wa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa kwenye maandamano yanayoongozwa na makamu mwenyekiti Taifa, Tundu Lissu.

Msafara wa Dk Biteko ulitokea nyuma ya msafara wa Chadema wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga na kukutana na wafuasi hao wa Chadema ambao waligoma kupisha msafara huo, hali iliyowalazimu polisi kutumia nguvu kutuliza ghasia za wafuasi wa Chadema.

Baada ya mzozo wa muda mfupi, msafara wa Dk Biteko ulipisha njia na kuchepukia pembeni na kuwaacha Chadema wakiendelea na safari yao.

Akizungumzia hali hiyo, Lisu amesema, "Naomba niwaambie, hii barabara ni ya maandamano, asitokee mtu nyuma kutuingilia, sitaki kuchokozwa." amesema kwa kifupi huku akishangiliwa na wafuasi wa Chadema.

View this post on Instagram

A post shared by Mwananchi (@mwananchi_official)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live