Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpinzani wa Nyalandu uchaguzi Chadema ataka kiongozi atakayewavusha 2020

86713 Pic+nyalandu Mpinzani wa Nyalandu uchaguzi Chadema ataka kiongozi atakayewavusha 2020

Mon, 2 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alphonce Mbasa amewataka wanachama wa chama hicho kuchagua viongozi wa kanda hiyo watakaowavusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba Mosi, 2019 katika mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa kanda hiyo unaofanyika mjini Dodoma.

Wanaowania uenyekiti ni Mbassa na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Mbassa amesema imebaki miezi sita kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu na kuwataka wajumbe kuchagua watu watakaowavusha.

"Mimi nimefukuzwa kazi mara nne, nimeacha mshahara wa Sh2.4 milioni lakini nitakubali nikishindwa (kwenye uchaguzi) nitaendelea kuwa mwanachama. Nina uchungu na Chadema maana ni chama kilichonilea,” amesema.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema ( Bavicha) Patrick Ole Sosopi ametaka wajumbe wa mkutano huo kuwachagua viongozi watakaokuwa chachu ya mabadiliko katika kanda ya kati, kuonyesha ukomavu kwa kufanya maamuzi yenye busara.

“Baada ya uchaguzi adui yetu ni CCM na si baina yetu," amesema Sosopi ambaye ndio msimamizi  wa uchaguzi huo akisaidiana na katibu wa baraza hilo, Julius Mwita.

Kanda ya kati ya chama hicho inajumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro.

Chanzo: mwananchi.co.tz