Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpina aibana Serikali ujenzi Bwawa la Mwalimu Nyerere

Luhaga Mpinaaaaaaaa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameendelea kuing'ang'ania Wizara ya Nishati kuhusu mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Julius Nyerere safari hii alitaka iundwe tume ya kuchunguza.

Mpina ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 20, 2022 bungeni wakati akichangia hoja ya bajeti kuu ya serikali.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kuzungumzia ujenzi wa bwawa hilo akidai kutoridhishwa na mwenendo wake.

Mbali na uchunguzi wa ujenzi wa bwawa hilo, ameomba Bunge liunde tume kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta na mbolea.

Katika mchango bungeni leo Juni 20, 2022, waziri huyo wa zamani wa Mifugo na Uvuvi amemwambia Spika, Dk Tulia Ackson kuwa akiunda tume kuchunguza mambo hayo, hatamsahau kabisa katika maisha yake.

"Naomba kukupa ushauri ambao hutakaa unisahau Katika maisha yote, naomba uunde tume kuchunguza ucheleweshaji wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere. Unda tume ichunguze kupanda Kwa bei za mafuta pamoja na sababu za vita, unda tume ichunguze kupanda bei ya mbolea, utakuja kunikumbuka," amesema Mpina.

Katika mchango wake mbunge huyo amezungumzia uamuzi wa serikali kutaka kubadilisha matumizi ya shamba la mifugo la lanchi ya Kongwa kuwa shamba la alizeti kwamba hayaonyeshi umuhimu wa kuwajali wafugaji.

Amebainisha kuwa maeneo mengi ikiwemo Mkoa wa Tabora ambako wangeweza kufyeka na kulima lakini kuing'ang'ania Kongwa ni uamuzi unaopaswa kupingwa na wabunge wote.

Chanzo: Tanzania