Dar es Salaam. Aisha Juma (19) ambaye ni mpamba video za wasanii (video vixen) nchini Tanzania na mwenzake wameikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kusambaza picha za ngono katika mitandao ya kijamii na kulawiti.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Samwel Philemon (34) mkazi wa Kigamboni.
Wamefikishwa mahakamani leo Jumatatu Februari 17, 2020 na kusomewa kesi ya jinai namba 24/2020 mbele ya Hakimu Mkazi, Rashid Chaungu.
Wakili wa Serikali, Kija Luzungana amedai Desemba 12, 2019 jijini Dar es Salaam, Aisha anadaiwa kusambaza picha za ngono kinyume na sheria ya mtandao.
Kija amedai shtaka la pili la kulawiti linamkabili Philemon anayedaiwa siku ya tukio alimuingilia Aisha kinyume na maumbile na kujipiga picha, kisha kuzisambaza wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria.
Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao walikana na upande wa mashtaka kudai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Pia Soma
- Sauti za Busara yaungana na CRDB kutangaza utalii Zanzibar
- Mkazi Tanga akamatwa na gramu 500 za dawa za kulevya
- Virusi vya corona vyaua zaidi ya 1,700
Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Februari 26, 2020.