Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohamed Ali mwenyekiti mpya UVCCM Taifa

Ali Mohammed Sd Mohamed Ali mwenyekiti mpya UVCCM Taifa

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamemchagua Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.

Kawaida ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja anachukua nafasi ya Kheri James ambaye Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Kawaida amepata kura 523 akiwashinda Farid Mohammed Haji aliyepata kura 25, Kassim Haji Kassu kura 2 na Abdallah Ibrahim Natepe aliyepata kura 1.

Akitangaza matokeo hayo Jumapili Novemba 27, 2022 Jijini Dodoma msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alimtangaza Kawaida kuibuka na ushindi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live