Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Farah ajitoa Uenyekiti CCM Babati

CCM Babati.jpeg Mo Farah ajitoa Uenyekiti CCM Babati

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: Tanzaniweb

Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, kwa mwaka 2010 hadi 2015 Mohamed Farah maarufu kama Mwanamaombi amejitosa rasmi kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Babati mjini.

Farah amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kukabidhiwa na Katibu wa CCM wa wilaya ya Babati mjini Daniel Muhina jana jumamosi ya Julai 2.

Hata hivyo, Farah hakuwa na maneno mengi wakati wa kuchukua fomu zaidi ya kusema ametumia haki yake ya kidemokrasia ya chama hicho ya kugombea nafasi hiyo.

"Ni kweli kama mlivyoona nimechukua fomu ya kuomba kupitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati mjini zaidi ya hayo sina mengine ya kuzungumza," amesema Farah.

Katibu wa CCM wilaya ya Babati mjini, Daniel Muhina amesema fomu zinazochukukiwa ni kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa wilaya na katibu wa siasa na uenezi wa wilaya.

Mhina ametaja fomu nyingine atakazotoa ni za wajumbe watatu wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, wajumbe 10 wa halmashauri Kuu ya CCM wilaya na wajumbe wawili wa mkutano mkuu wa CCM mkoa.

"Fomu zimeanza kutolewa Julai 2 na mwisho ni Julai 10 ila wagombea wanakumbushwa hakuna mbwembwe wala maandamano wakati wa kuchukua na kurudisha fomu," amesema Muhina.

Hata hivyo, Muhina amesema kwa sasa hawezi kutaja majina ya wanachama wa CCM waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali zilizotangazwa.

Chanzo: Tanzaniweb