Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyika atimkia Marekani.

Mnyika Mnyikaa Amsha Amsha.jpeg John Mnyika.

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, yuko nchini Marekani katika ziara ya kikazi ya siku nne, itakayoanza tarehe 4 hadi 7 Desemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya ziara hiyo  imetolewa jana tarehe 3 Desemba 2023 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema.

Taarifa ya Mrema ilisema kuwa, Mnyika atafanya mambo mawili akiwa ziarani, la kwanza likiwa ni kuhudhuria jukwaa la mwaka la Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU), lenye lengo la kujadili na kutoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani.

Jambo la pili ambalo Mnyika atalifanya katika ziara hiyo, ni kufanya majadiliano na mashirika mbalimbali ya kimataifa yenye makao makuu yake jijini Washngton, nchini humo.

“Katibu Mkuu ameondoka nchini  tarehe  3 Desemba 2023, alfajiri kuelekea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku nne. Akiwa Jijini Washington, atahudhuria jukwaa la mwaka la IDU litakalohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali duniani,” ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live