Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyika asisitiza mabadiliko ya Katiba kufikia demokrasia

Mnyika 1 Mnyika asisitiza mabadiliko ya Katiba kufikia demokrasia

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema Watanzania wanahitaji Katiba mpya itayokuwa na maudhui ya wananchi wote.

Hayo ameyasema leo Ijumaa Agosti 12, 2022 wakati akizungumza kwenye kongamano la Baraza la Vijana wa chama hicho, lililofanyika kitaifa mkoani Shinyanga leo, ambapo amesema vijana wote wanatakiwa kuwa na lugha moja ya kudai suala hilo.

"Ili Tanzania tupate uchaguzi huru wa haki ni vizuri tusimamie katiba mpya ili tuweze kupata bunge huru, hivyo viongozi wote wa Chadema tunatakiwa tuongeze nguvu ili tuwe na tume huru na katiba mpya na tuongeze zoezi la usajili wa chama," amesema Mnyika.

"Lengo kubwa la kufanya kongamano hilo ni kutaka katiba mpya na kudai tume huru, tuutumie uchaguzi wa ndani ya chama kuanzia vitongoji na vijiji, ili kuhakikisha CCM madarakani, kwani bila kuiondoa CCM madarakani Tanzania itaendelea kukwama," amesema Mnyika.

Aidha Mnyika amesema Vijana wote ambao wanatarajia kuwa viongozi ndani ya Chadema waanze kuwekeza ndani ya chama kwa sababu kauli mbiu yetu inasema vijana ni Taifa la leo.

"Rais alisema kuwa kushuka kwa mafuta ni mpaka vita viishe, kama rais hatataka kushusha bei ya mafuta ashuke kwenye kiti hicho apandishwe mtu anayeweza kukaa kwenye kiti hicho na kushusha mafuta," amesema Mnyika.

Amewataka vijana wa kike na wakiume wajitokeze kugombea kwenye serikali za mtaa ili waweze kutetea Taifa lao na kuwa mstari wabele katika kuongoza.

Naye Naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu amesema wanataka katiba mpya ikazalishe mambo mbalimbali ikiwemo serikali tatu.

"Baadhi ya watu wanasema ni gharama kuwa na serikali tatu,  lakini hakuna gharama zinazoongezeka kwa sababu zanzibar kuna makamu wa rais na huku kuna makamu wa Rais Zanzibar kuna Jaji mkuu na huku kuna jaji mkuu  hivyo hakuna kitakachoongezeka," amesema Mwalimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live