Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyika asema Kikosi kazi kimepotosha mchakato wa Katiba

MNYIKA123 Mnyika asema Kikosi kazi kimepotosha mchakato wa Katiba

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema ripoti ya Kikosi Kazi kimepotosha mchakato wa Katiba kwa kutaka Rasimu ya Katiba maafuru kama Rasimu ya Jaji Joseph Warioba ipelekwe moja kwa moja kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Ameyasema hayo jana Oktoba 26 katika mjadala wa ripoti ya Kikosi Kazi uliondaliwa na Mwananchi Communications Ltd kupitia Twitter Space, ambapo amesema ripoti hiyo imekopa suala la muundo wa Tume ya Uchaguzi kutoka kwenye Katiba inyopendekezwa.

“Tulikuwa hatukubalianana muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kama tungebaki hadi dakika za mwisho ni sehemu ambayo tusingekubaliana nayo,”

“Katika muundo mzima wa uchaguzi pendekezo limeeleza uchaguzi uendelee kusimamiwa na watumishi wa umma, kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa haijaonyesha usimamiwe na nani

“Chakushangaza kikosi kazi kueleza uchauzi uendelee kusimamiwa na Tamisemi wameshindwa kwenda kwenye muelekeo wa namna gani uchaguzi uendelee kuwa huru na wa haki,” amesema Mnyika

Chanzo: mwanachidigital