Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyika alia utekelezaji wa mapendekezo Tume ya Nyalali

MNYIKA WEB John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha (Chadema), John Mnyika amesema kama mapendekezo ya Tume ya Jaji Francis Nyalali yangefanyika baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, vyama vya upinzani vingefanya vizuri zaidi.

Mnyika amesema hayo jana Alhamisi Septemba 16, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya demokrasia ambayo iliwakutanisha wadau mbalimbali kujadili miaka 30 ya demokrasia ya Tanzania.

Alisema Tume ya Nyalali ilipendeke za mabadiliko ya Katiba pamoja na sheria 40 ili ziendane na mazingira ya mfumo wa vyama vingi.

Hata hivyo, alisema watawala walikataa kutekeleza hilo kwa kuhofia kwamba wangepoteza dola. Aliwataka Watanzania kuendelea kupigania katiba mpya kwa sababu ndiyo mkombozi.

“Mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali yangetekelezwa mwaka 1995, na kama katiba mpya ingeandikwa wakati ule, matokeo ya uchaguzi yasingekuwa vile yalivyokuwa.

“Huwezi ukasema nchi ina demokrasia wakati vyama haviwezi kufanya hata mikutano ya hadhara. Tunahitaji kujenga mifumo na taasisi imara,” alisema Mnyika.

Mbunge huyo wa zamani alisema Tanzania haijawahi kukubali demokrasia ya vyama vingi yenye demokrasia ya haki kwa sababu watawala hawataki wakidhani kufanya hivyo watapoteza dola.

“Mfumo wa vyama vingi ulitolewa kama zawadi na CCM. Wakati wowote mfumo wa vyama vingi unaweza kuondolewa kama ilivyokuwa mwaka 2020,” alisema Mnyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live