Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema Serikali inakwepa kutoa tathimini ya kwa nini idadi ya wapiga kura inapungua nchini, ila kwa tafiti walizofanya, wamegundua wananchi wamepoteza imani na mifumo ya uchaguzi nchini.
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema Serikali inakwepa kutoa tathimini ya kwa nini idadi ya wapiga kura inapungua nchini, ila kwa tafiti walizofanya, wamegundua wananchi wamepoteza imani na mifumo ya uchaguzi nchini. Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) leo Jumatatu Machi 11, 2024, Mnyika amesema: "Tukitaka kuongeza idadi ya wapiga kura imani katika mifumo ya uchaguzi iongezeke, tudai Katiba mpya na marekebisho ya sheria.Lazima tutengeneze uwanja sawa wa kiuchaguzi hayo yatatengeneza mwamko wa mabadiliko.’’