Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi wa uchaguzi Korogwe apokea rufaa ya Chadema

13352 Chaguzi+pic

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rufaa ya mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe (Chadema) Amina Saguti imepokewa na Kaimu Mkurugenzi wa uchaguzi Wilaya ya Korogwe, Florian Kimaro.

Katika rufaa hiyo, Saguti anapinga uamuzi wa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM Timotheo Mzava kuwa amepita bila kupingwa.

Taarifa iliyotolewa leo Agosti 22 na Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene imedai kuwa uteuzi wa Saguti umewekewa vikwazo baada ya msimamizi wa uchaguzi kukataa kupokea fomu yake leo mchana.

“Mgombea huyo akiambatana na viongozi wa Chadema Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo,” imesema taarifa hiyo.

Imesema Chadema kimemwandikia Mkurugenzi wa NEC, Athuman Kihamia na kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe ikiwamo kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz