Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa kigogo CHADEMA aitwa Mahakamani

Capture (600 X 244) Mke wa kigogo CHADEMA aitwa Mahakamani

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano na Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene, Susanne Masele ameamriwa kuhudhuria katika Mahakama ya Mwanzo Kimara kwa ajili ya shauri la madai ya talaka lililofunguliwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Temeke.

Susanne Masele ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2015 - 2020), ameitwa Mahakamani hapo kufuatia shauri la madai namba 1085 la mwaka 2022 lililofunguliwa na Mdai Makene dhidi ya Mdaiwa Susanne.

Tangazo la Mahakama la kumuamuru Susanne afike Mahakamani hapo limeibainisha kuwa; “Wewe Susanne Peter Masele popote pale ulipo unaamuriwa na Mahakama hii kuhudhuria hapa Mahakamani mnamo 30/08/2022, kama hutahudhuria basi Mahakama hii itasikiliza upande mmoja na uamuzi kutolewa”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live