Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miradi ya NHC Kawe na Moroco yaibuka Bungeni

Makoa Makoa akiwa bungeni

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Serikali kuchukua hatua stahiki na kwa wakati, ili kuiwezesha Shirika la Nyumba Nchini (NHC) kukamilisha miradi minne mikubwa ya jijini Dar es Salaam ili tija ya uwekezaji huo ionekane.

Ally Makoa ameitaja miradi hiyo kuwa ni Morocco Square, Seven Eleven - Kawe, Golden Premier Residence - Kawe na Plot 300 Regent Estate Mikocheni iliyopo Dar es Salaam.

Amesema kwa muda mrefu sasa miradi hiyo imesimama, tangu ujenzi wake ulipoanza mwaka 2012 na 2013 kwa fedha za mkopo ambapo miradi hiyo ilitarajiwa kukamilika mwaka 2015 na 2016.

“Kutokamilika kwa miradi hiyo kwa wakati kumeongeza gharama za ujenzi, ongezeko la riba, na Serikali kupata hasara kubwa ambayo inasababisha kutopatikana kwa thamani halisi ya fedha iliyowekezwa,”amesema.

Ameitaka Serikali kuchukua hatua stahiki na kwa wakati ili kuiwezesha Shirika hilokukamilisha miradi hiyo ili tija ya uwekezaji huo ionekane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live