Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milioni 63/- zakamilisha ujenzi wa Ofisi Mpya ya CCM Sengerema

A2 1024x768 Ccm Sengerema Milioni 63/- zakamilisha ujenzi wa Ofisi Mpya ya CCM Sengerema

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema iliyokuwa imekwama kumalizika kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita hatimaye imekamilika kutokana na michango ya wananchi sambamba za wafadhiri toka ndani ya chama hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Mhusin Zikatimu alipokuwa akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema jitihada za kukamilika kwa jengo hili zimefanywa na mwenyekiti wa CCM Marco Makoye anayetetea nafasi kwa kujitoa kwa hali na mali kwa kushirikiana na wana-CCM kuhakikisha ofisi hii inakamlika.

Zikatimu amesema ofisi hiyo ambayo kwa sasa imekamilia itaanza kutumika rasmi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa chama na hivi sasa shughuri ndogondogo zinafanyika.

“Nawaomba wanaCCM waone jitihada zinazofanywa na viongozi wao kuhakikisha chama kinasonga mbele” amesema zikatimu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM marco Makoye anayetetea nafasi yake amesema kukamilika kwa ofisi hii kumetokana na jitihada za wanachama wote wa chama cha mapinduzi kwa kujua umuhimu wa kuwajibika .

"Leo (juzi) ninajivunia kupata ofisi mpya CCM hivyo nifuraha kwetu kama wanaCCM” amesema Makoye.

Mmoja wa wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo, Amina Juma amesema ofisi hiyo ambayo iliwashinda wenyeviti wa awali hadi wakahukumiwa na kura za wanaCCM, sasa imekamilika heko zimwendee mwenyekiti Marco Makoye kwa kuwaunganisha wanaCCM na ofisi imekamilika.

Jengo la ofisi ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema lililokuwa limetelekezwa kwa miaka 15 hatimaye limekamilika na liko mbioni kutumika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live