Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikutano ya kampeni uchaguzi wa serikali za mitaa wabainishwa

72739 Pic+mikutano

Sat, 24 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mikutano ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania utakaofanyika Novemba 24,2019 zitaanza saa 2.00 asubuhi na kumalizika saa 12.00 jioni.

Hayo yamo katika kanuni za uchaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa zilizotolewa jana Ijumaa Agosti 23,2019 na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo.

Kanuni hizo zinasema pia  mgombea ama mwakilishi wa mgombea au chama cha siasa anaweza kuitisha na kuhutubia mkutano wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya mikutano ya kampeni iliyoandaliwa na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).

Pia, kanuni hizo zimesema wagombea na vyama vya siasa hawatarudi wa kuendesha kampeni kwa kutumia rushwa, kutoa maneno ya kashfa au lugha za matusi.

Kanuni hizo zinasema hawataruhusiwa kufanya ubaguzi wa jinsia, maumbile, ulemavu, dini, rangi kabila au ubaguzi mwingine wowote au kutoa maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani au kusababisha vurugu.

"Mgombea yeyote ambaye hakuridhika na matokeo ya uchaguzi au uendeshaji wa uchaguzi atakuwa na haki ya kufungua shauri katika mahakamani ya Wilaya ndani ya siku 30 tangu siku ya kutangaza matokeo ya uchaguzi,” zinaeleza kanuni hizo

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz