Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikataba CCM kufumuliwa

55743 CCM+PIC

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema wameanza kupitia upya mikataba ya mali za chama hicho kiliyoingia na wawekezaji ambayo imekuwa ikilalamikiwa.

Dk Bashiru aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari mjini hapa juzi kuwa baada ya kukamilisha upitiaji watachukua hatua kutokana na kubaini kuwepo kwa ufisadi.

Akitoa mfano wa mikataba hiyo, alisema ni ule wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) lilipo katika makutano ya barabara za Lumumba na Morogoro pamoja na na jengo la Umoja wa Wanawake (UWT) lililopo Morocco, yote yakiwa jijini Dar es Salaam.

Alisema majengo hayo yamebeba mikataba ya kinyonyaji na kibaguzi, kwani wawekezaji wake walichukua hati za jumuiya hizo na kwenda kukopea fedha, lakini ajabu ni kwamba jumuiya zinalipwa asilimia 25 wakati wanaojiita wawekezaji wanachukua 75.

Dk Bashiru alisema CCM imefanikiwa kudhibiti mapato yake na kuwa na akiba ya Sh7 bilioni, huku akitolea mfano wa moja ya wilaya kuwa ilikuwa na makusanyo ya Sh6 milioni, lakini sasa yamefikia Sh400 milioni. Hata hivyo, hakuitaja wilaya hiyo.

“Kutokana na matumizi ya mfumo wa kisasa, hivi sasa naona fedha zote zinazoingia katika chama na kutoka, ada za wanachama zilikuwa hazionekani lakini sasa unaweza hata kufuatilia ada iliyolipwa,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz