Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka mitatu ya Mwinyi, matanki ya maji yaongezeka

Rais Mwinyi Amteua Naibu CAG.jpeg Miaka mitatu ya Mwinyi, matanki ya maji yaongezeka

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi serikali kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imeanza kukamilisha kwa miradi mikubwa ya Maji ikuhusisha Matanki ya kuhifadhia maji kutoka matanki 64 madogo yanayohifadhi maji lita Milioni 46.2 na kufikia ujenzi wa matanki makubwa 25 Za Uviko 19 pamoja na matanki ya miradi wa Exim yenye jumla ya ujazo wa Lita Milioni 144

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Mhandisi Dkt. Salha Mohammed Kassim wakati akielezea mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa Rais Mwinyi.

Dkt Salha amesema ZAWA inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhia Maji 25 pamoja na visima vipya 102 ambayo kwa pamoja vitakuwa na uwezo wa kuzalishaji Maji Zaidi ya Lita Milioni Mia tatu na arobaini na tano katika maeneo yote ya Unguja na Pemba

Sambamba na hatua hiyo amesema tayari shughuli za usambazaji wa mabomba ya kusafirishaji maji imeanza na baadhi ya maeneo tayari miradi hiyo imeshaanza kufanya kazi na kuondosha changamoto ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama visiwani Zanzibar

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Mwinyi, sekta ya maji imekua ni moja ya sekta muhimu iliyopewa kipaumbele kwa kuiwezesha kifedha na kitaaluma ili kufanikisha miradi hiyo ambayo kwa ujumla itagharimu zaidi ya Bilioni Mia mbili za Kitanzania na kufanikisha usambazaji wa huduma hiyo katika maeneo yote ya Unguja na Pemba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live