Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mh. Zitto kufanya ziara Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Chama cha ACT- Wazalendo kupitia Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho wameanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.



Zitto kupitia taarifa yake aliyoitoa leo, imeeleza kuwa lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi na kushiriki kazi za maendeleo katika Kata hizo.

Leo, nikiwa pamoja Na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, Mama Annamarrystella Mallack, Katibu wa Kamati hiyo, ndugu Janeth Joel Rithe, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti, ndugu Emmanuel Mvula tumeanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama chetu cha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi, kushiriki kazi za maendeleo katika kata, kuzungumza na kamati ya maendeleo ya kata, kuzungumza na wananchi wa kata husika, kuangalia utendaji wa madiwani kutokana na matarajio ya wananchi, kuona vikwazo na changamoto za Madiwani wetu, kusisitiza Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote ya Kata, pamoja na kufanya tafiti juu ya masuala ya kisera pamoja na miradi ya maendeleo ambayo ACT Wazalendo Taifa tunaweza kuyabeba kusaidia madiwani wetu.

Ziara itafanyika kwa siku 19 katika mikoa 8 husika, ambako leo tumeanzia Kata ya Kiparang’anda, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo

Kiparang’anda

Mkuranga

Pwani

Februari 19, 2018

Chanzo: bongo5.com