Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea wa SAU aibukia mkutano wa Chadema

10202 SAU+PIC TanzaniaWeb

Sun, 5 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mgombea Udiwani kata ya Mawenzi kwa tiketi ya chama cha Sauti ya Umma (Sau), Issack Kireti jana alikuwa kivutio cha aina yake baada ya kuibuka katika mkutano wa Chadema.

Kireti ambaye ahadi zake katika kampeni hizo zimekuwa zikiwavunja mbavu wananchi, aliibuka katika mkutano huo saa 11:30 alasiri, wakati Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini akihutubia.

Selasini ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa Chadema mkoa Kilimanjaro, alikuwa akimnadi mgombea udiwani wa chama hicho katika kata ya Mawenzi, Afrikana Mlay, anayechuana vikali na, Apaikunda Naburi wa CCM.

“Nimekuja kusikiliza sera zao ili nione kama ni nzuri, nikiona nzuri nitazichukua ili nizitumie nikitekeleza majukumu yangu kama diwani kwa sababu mimi ndio diwani mtarajiwa. Hakuna mwingine,” alisema.

Kireti aliliambia gazeti hili kuwa hata Rais John Magufuli, ziko sera nzuri za Chadema ambazo walihubiri mwaka 2015 ambazo amezichukua ikiwamo suala la mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Akihutubia katika mkutano huo, Selasini aliwataka polisi kuacha kutumika kurekodi mikutano ya Chadema badala yake wawaeleze wananchi juu ya matukio ya kupotea kwa wananchi.

“Waache kuja hapa na kuturekodi ili kuwapelekea wakubwa wao wanaowatuma. Watueleze Ben Saanane yuko wapi. Ni mara ya kwanza nchini tunaona maiti kwenye viroba,” alidai Selasini.

Selasini alienda mbali na kudai kuwa Rais Magufuli hana uwezo wa kufuta upinzani Kilimanjaro kwani ulikuwapo hata kabla ya uhuru na maendeleo ya kaskazini yaliletwa na wananchi wenyewe.

Chanzo: mwananchi.co.tz