Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea wa Chadema Ukonga huyu hapa

11522 CHADEMA+2+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ilala, Dk Makongoro Mahanga amemtangaza Asia Msangi kuibuka mshindi katika kura za maoni kumsaka  mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Ukonga.

Hata hivyo, amesema kamati kuu Taifa ndiyo itakayotoa baraka za mwisho kwa mgombea huyo baada ya kuchambua majina yote.

Akitangaza matokeo ya kura ya maoni leo Jumapili Agosti 12, 2018, Dk Mahanga amesema Asia ameibuka mshindi baada ya kupata kura 91 sawa na asilimia 64.

Uchaguzi jimbo la Ukonga unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema, Mwita Waitara kujiuzulu na kujiungana na CCM.

Katika ufafanuzi wake Dk Mahanga amesema wajumbe waliopiga kura walikuwa 141 kati ya 158 waliopaswa kupiga kura hizo.

Amesema wagombea wengine na idadi ya kura walizopata katika mabano ni Swea Rajabu (21) ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema katika jimbo hilo pamoja na Thomas Nyahende aliyepata kura 29.

“Kamati kuu Taifa haifungwi na ile hoja ya mshindi namba moja aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa jimbo la Ukonga. Kamati Kuu itachagua mtu atakayefaa," amesema Dk Mahanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz