Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea wa Chadema Ukonga atamba hanunuliki

15863 Pic+chadema+ukonga TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea ubunge wa Chadema Ukonga, Asia Msangi amesema yeye ni mwanamke shupavu na hanunuliki huku akibainisha kuwa kiongozi mzuri ni yule asiyekuwa na tamaa.

“Ninawahakikishia wakazi wa mtaa wa Mwanagati kata hii ya Mzinga. Mimi siwezi kununuliwa,” amesema Asia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jioni Jumatano Septemba 5, 2018 katika kata hiyo.

Amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wa Chadema kuhakikisha wananchi wa Ukonga wanapata maendeleo.

Kwa upande wake diwani wa Sombetini mkoani Arusha, Ally Malanga amewataka polisi kuhakikisha wanalinda usalama siku ya uchaguzi Septemba 16, 2018.

“Hawa polisi ni rafiki zetu hivyo tusiwaogope tuna imani watasaidia kulinda kura hawatatupiga mabomu,” amesema.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema, Mwita Waitara kukihama chama hicho na kujiunga na CCM, ambako amepitishwa kuwania nafasi hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz