Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea wa Chadema Ukonga aja na mpya

16055 Kampeni+pic TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea wa Chadema jimbo la Ukonga, Asia Msangi amesema wapinzani wake wameanza kuchana mabango yake, kubainisha kuwa hatua yao hiyo haiwezi kumfanya akose kura za wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Buyuni Chanika leo jioni Alhamisi Septemba 6, 2018, Asia amesema anachojivunia kwa sasa ni kukubalika kwake na wananchi wa Ukonga, kutamba kuwa atashinda kwa kura nyingi dhidi ya wagombea wengine, akiwemo Mwita Waitara wa CCM.

Amewataka wananchi wamchague ili awaletee maendeleo, huku akimponda Waitara kuwa hakufanya lolote alipokuwa mbunge wa Ukonga kuanzia mwaka 2015 hadi Julai, 2018.

“Watu wanasema eti nitanunuliwa, haliwezi kutokea hilo na kamwe siwezi kuwasaliti wananchi wangu. Mimi nipo kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Ukonga," amesema Msangi.

Amewataka wananchi kutokata tamaa kutokana na wapinzani kutoibuka na ushindi katika chaguzi ndogo zilizopita, kubainisha kuwa hali itakuwa tofauti katika jimbo la Ukonga.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Septemba 16, 2018 siku ya kupigakura na kumchagua yeye, kujifananisha na mbunge wa chama hicho jimbo la Kawe, Halima Mdee.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz