Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea udiwani ‘aponda’ wasiotaka achaguliwe

1dade0495732ca00d158e24bb21477c1.jpeg Mgombea udiwani ‘aponda’ wasiotaka achaguliwe

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Karema (CCM) katika Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Michael Kapata amewaomba wakazi wa Kata hiyo wamchague tena na wawapuuze wanaotaka anyimwe kura kwa sababu ameongoza muda mrefu.

Alitoa kauli hiyo katika kampeni ya uchaguzi iliyozinduliwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi, Beda Katani katika Jimbo la Mpanda Vijijini Kata ya Karema.

"Wapo baadhi ya wakazi wa Kata ya Karema wanaonichukia kwa kuwa Diwani wa Kata hii kwa miaka 15 mfululizo; wanashawishi nisichaguliwe tena eti nimehudumu kwa kupindi kirefu...” alisema.

Akaongeza: “Kuongoza kwa muda mrefu siyo sababu ya msingi ya kuwafanya msinipigie kura .... Mbona hata mke wangu nimeishi naye kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 30, lakini hamjanilalamikia na kutaka tuachane?" Alihoji Kapata.

Aliomba wakazi hao wasiangalie muda alioongoza, bali waangalie namna alivyoshirikiana nao kuwapelekea maendeleo kupiria uongozi wake wa miaka 15.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini, Selemani Kakoso anayetetea nafasi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo, aliwaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimewaletea maendeleo makubwa.

Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi, Katani alisema wana matumaini makubwa wananchi hawatawaangusha kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 kwa kuwa chama hicho kimetekeleza vizuri ilani yake.

Chanzo: habarileo.co.tz